NEWS

Wednesday, 18 January 2023

RPC Tarime Rorya awakumbusha wamiliki wa vituo vya mafuta mambo 12 ya kuzingatia



Na Mwandishi Wetu, Tarime
----------------------------------------

KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Polisi Tarime Rorya, ACP Geofrey Sarakikya (pichani), amekutana na wamiliki wa vituo vya mafuta mkoani humo na kuwakumbusha mambo 12 ya kuzingatia katika uendeshaji wa biashara hiyo.

Kikao hicho kilifanyika mjini Tarime hivi karibuni, ambapo pia kilihudhuriwa na maofisa wakaguzi wa polisi, mameneja na watumishi wa vituo vya mafuta.

RPC Sarakikya alimkaribishwa na Mnadhimu Mkuu Namba Moja ACP Ame Anoqie kufungua kikao hicho na kuwajulisha wajumbe kuwa lengo ni kuwakumbusha wamiliki wa vituo vya mafuta na watumishi wao kuhusu usalama wa maeneo yao ya kazi.

Baadaye RPC Sarakikya aliekeza wamiliki wote wa vituo vya mafuta katika wilaya za Tarime Rorya kuhakikisha wanazingatia mambo 12 yafuatayo:

Kufunga kamera za CCTV zenye ubora camera ili kuweza kuwabaini wanaotenda uhalifu katika vituo vyao vya mafuta na maeneo yaliyo jirani.

Kuhakikisha vituo vya mafuta vina ulinzi thabiti na wamiliki kufanya ufuatiliaji wa walinzi na wafanyakazi wanaowaajiri.

Wamiliki kuhakikisha wanajenga uzio imara katika Vituo vya Mafuta, lakini pia kuhakikisha watumishi wanaokusanya fedha hawakai na fedha za mauzo kwa muda mrefu bila kuziwasilisha kwenye hifadhi madhubuti.

Wamiliki kutokuruhusu vyombo vya moto kupakia na kushushia abiria katika vituo vya mafuta, lakini pia kutokuruhusu waendesha pikipiki (boda boda) kuegesha kwenye maeneo ya vituo hivyo.

Wamiliki kuchukua tahadhari ya majanga ya moto kwa kuweka vifaa vya kuzima moto na kukata bima ya vituo vya mafuta.

Wamiliki kuwa makini wanapoingia mikataba ya ulinzi na kampuni binafsi za ulinzi, ikiwa ni pamoja na kuzingatia taratibu zote za ulinzi na uaminifu kwa walinzi wao.

Wamiliki kutambua kuwa Jeshi la Polisi lina wajibu wa kufanya doria na ukaguzi katika vituo vya mafuta mara kwa mara.

Wamiliki wa vituo vya mafuta kujenga ushirikiano baina hao na kuwa na mawasiliano na Jeshi la Polisi.

Aidha, RPC Sarakikya aliwapa wamiliki wa vituo vya mafuta namba za simu za viongozi wa Polisi Mkoa na Wilaya, kwa ajili ya kutoa taarifa za matishio ya uhalifu na mienendo inayotiliwa mashaka.

Wamiliki wote wa vituo vya mafuta waliohudhuria kikao hicho walikubali na kuahidi kutekeleza maelekezo hayo ya RPC Sarakikya.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages