NEWS

Wednesday 4 January 2023

Wanafunzi Shule ya MOREGAS wapiga A na B mtihani wa marudio wa darasa la saba



Na Mara Online News
-----------------------------------

WANAFUNZI wa Shule ya Msingi MOREGAS English Medium waliorudia Mtihani wa Taifa wa Kuhitimu Darasa la Saba Mwaka 2022, wamepata ufaulu mnono wa madaraja A na B, kwa mujibu wa matokeo ya mtihani huo yaliyotangazwa na Baraza la Taifa la Mitihani Tanzania (NECTA) leo Januari 4, 2023.

Matokeo hayo yanaonesha kuwa wanafunzi wa Shule ya MOREGAS wapatao 45 walifanya mtihani huo wa marudio, ambapo kati yao, 27 wakiwemo wasichana 12 na wavulana 15 wamepata ufaulu wa daraja A, wengine 17 (wasichana wanne na wavulana 13) wamepata daraja B na mmoja daraja C.

Kaimu Katibu Mtendaji wa NECTA, Athumani Amasi, amesema wanafunzi hao ni kati ya 2,180 waliofanya mtihani huo wa marudio kati ya Desemba 21 na 22, 2022.

Mkurugenzi wa Shule ya Msingi MOREGAS English Medium, Cosmas Mseti, ameeleza kupokea matokeo hayo kwa furaha.

“Sisi tumepokea matoke vizuri na tunaomba wazazi na walezi kuendelea kuiamini shule yetu - itaendelea kufanya kizuri kama ilivyo kawaida yetu,” amesema Mseti katika mazungumzo na Mara Online News, muda mfupi baada ya matokeo hayo kutangazwa na NECTA.

Mkurugenzi wa Shule ya Msingi MOREGAS English Medium, Cosmas Mseti.

Shule ya Msingi MOREGAS English Medium ipo eneo la Majengo Mapya katika mji mdogo wa Sirari wilayani Tarime, Mara.

Nayo Shule ya Msingi Mugini iliyopo Magu mkoani Mwanza, imefanya vizuri katika mtihani huo wa marudio, baada ya wanafunzi wake 41 kufaulu kwa madaraja A na B.

Kati ya wanafunzi hao 41, waliopata darajaa A ni 34 (wasichana 16 na wavulana 18), huku saba wakiwemo wasichana sita na mvulana mmoja wakipata ufaulu wa daraja B.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages