NEWS

Tuesday 10 January 2023

Wapanda miti kupendezesha mazingira jengo jipya la ofisi ya Kamanda Mkoa wa Polisi Tarime RoryaNa Mara Online News
----------------------------------

MNADHIMU Mkuu Namba Moja wa Mkoa wa Polisi Tarime Rorya, ACP Ame Anoqie (pichani juu kulia), ameongoza maafisa, wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali kupanda miti zaidi 70 katika eneo la jengo jipya la ofisi ya Kamanda ya mkoa huo lililopo Bomani - mjini Tarime.

Shughuli hiyo ilifanyika jana Januari 9, 2023 ambapo ilihusisha miti ya kivuli, maua na mapambo, ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Tanzania.

Aidha, ACP Anoqie ambaye liongoz shughuli hiyo kwa niaba ya Kamanda wa Polisi Mkoa (RPC) wa Tarime Rorya, ACP Geofrey Sarakikya, alielekeza itafutwe pia miti ya matunda ipandwe, akisisitiza kuwa pamoja na manufaa mengine, miti mbalimbali itawezesha hewa safi na kupendezesha mazingira ya jengo hilo.

Oktoba 3, 2022, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la ofisi ya Kamanda wa Mkoa wa Polisi Tarime Rorya.


Naibu Waziri Sagini ambaye pia ni Mbunge wa Butiama mkoani Mara, alieeleza kuridhishwa na ujenzi wa jengo hilo mbalo ni la kisasa kuwahi kushuhudiwa katika Jeshi la Polisi Tarime Rorya.

RPC Sarakikya alisema ujenzi wa jengo hilo lenye ghorofa mbili umegharimu shilingi bilioni 1.5 zilizotolewa na Serikali chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Kamanda huyo alisema kukamilika kwa ujenzi wa ofisi hiyo sasa utalipunguzia kama si kuliondolea Jeshi la Polisi Tarime Rorya adha ya kupanga kwenye majengo ya taasisi nyingine.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages