NEWS

Sunday 8 January 2023

Waziri wa mifugo ziarani Tarime Vijijini



Na Mwandishi wetu, Tarime
-----------------------------------------

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Dkt Mashimba Ndaki (pichani anayesaini), mapema leo Januari 8, 2023 amefanya ziara katika vijiji vya wilayani Tarime vilivyopo jirani na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

“Tayari Waziri amewasili Karakatonga kwa ajili ya kuhutubia mkutano wa wananchi,” amesema mwandishi wa Mara Online news.

Katika ziara hiyo, Waziri huyo mwenye dhamana ya sekta ya mifugo na uvuvi, amefuatana na Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Kanali Michael Mntenjele na Mbunge wa Tarime Vijijini, Mwita Waitara, miongoni mwa viongozi wengine.

Waziri Mashimba anatarajiwa pia kufanya mkutano wa hadhara katika kijiji cha Kengonga kilichopo kata ya Nyanungu, kwa mujibu wa Diwani wa Kata hiyo, Tiboche Richard.

Wananchi wa vijjiji hivyo wamekuwa wakilalamikia ukosefu wa maeneo ya malisho, huku baadhi yao wakijikuta matatani wanapokuwa wameingiza mifugo kuchunga katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, jambo ambalo linasababisha migogoro kati yao na wahifadhi.

Kulingana na Sheria za Tanzania, kuingiza ya mifugo ndani ya hifadhi za taifa ni kosa la jinai.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages