NEWS

Saturday 7 January 2023

Shirika la RAID lakubali mwaliko wa kutembelea Barrick North Mara



Na Mwandishi Wetu
---------------------------------

SHIRIKA la kutetea haki za binadamu la Rights and Accountability in Development (RAID), lenye makazi nchini Uingereza, limekubali mwaliko wa muda mrefu wa kutembelea Mgodi wa Dhahabu wa North Mara wilayani Tarime, katika wiki inayoanzia Januari 30, 2023.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo, Kampuni ya Barrick Gold imesema lengo ni kuionesha RAID miradi ambayo imefanywa na mgodi wa North Mara katika azma yake ya kuboresha maisha na ustawi wa jamii zinazouzunguka, kupata uelewa na uhalisia wa mazingira ya utendaji mgodini na kukutana na wadau wengine.

“Pia North Mara na RAID watazungumzia ripoti na mbinu za RAID na kutoa mapendekezo yanayofaa,” imesema taarifa hiyo.

Mgodi wa North Mara na wadau wengine wanatazamia kuwa na mazungumzo ya manufaa na timu nzima ya RAID, taarifa hiyo imehitimisha.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages