NEWS

Thursday 16 February 2023

Mchungaji afariki dunia Msumbiji akijaribu kufunga kwa siku 40 kufikia rekodi ya YesuMCHUNGAJI wa nchini Msumbiji amefariki dunia baada ya kufunga kwa siku 40 akijaribu kufikia rekodi iliyofikiwa na Yesu kwenye Mlima wa Mizeituni wa Biblia.

Kifo cha Francisco Barajah, mchungaji na mwanzilishi wa Kanisa la Kiinjili la Santa Trindade katika jimbo la kati la Manica, kilithibitishwa Jumatano wiki hii.

Alifariki dunia alipokuwa akitibiwa katika hospitali ya Beira ambako alihamishiwa akiwa katika hali mbaya.

Baada ya siku 25 za kufunga, alikuwa amepungua uzito sana kiasi cha kutoweza kusimama, kuoga au kutembea.

Siku kadhaa baadaye, kwa msisitizo wa ndugu na waumini, alipelekwa hospitalini lakini jitihada za kumrejesha kwenye afya hazikufaulu.

Waumini wa kanisa lake na majirani zake hawakushangazwa na mabadiliko hayo, kutokana na kupungua uzito na umbo lake kuharibika katika siku za hivi karibuni. BBC

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages