NEWS

Monday, 13 February 2023

Mchungaji wa Nigeria ahubiri kanisani akiwa amebeba bunduki aina ya AK-47




MCHUNGAJI mwandamizi wa Nigeria (pichani), alizua mjadala mpana katika mitandao mingi ya kijamii wikendi iliyopita, baada ya kubeba bunduki ya kivita wakati alipokuwa akihubiri kanisni.

Mchungaji huyo, Uche Aigbe wa Kanisa la House on the Rock mjini Abuja, alizua tafrani wakati wa ibada ya Jumapili alipopanda juu ya mimbari akiwa amebeba bunduki aina ya AK-47.

Hi haikuwa kawaida kutokana na ilivyozoeleka kuwa alipaswa kubeba biblia, mafuta ya upako, au bakuli ya maji matakatifu kama wahubiri wengi wanavyofanya wanaposimama juu ya mimbari.

Lakini ni kwanini Mchungaji Uche alibeba bunduki aina ya AK47 kanisani?

‘Chunga Imani yako’
Hii ndiyo iliyokuwa mada kuu ya mahubiri ya Jumapili, kulingana na kile kanisa lilichapisha kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Kwa hivyo Mchungaji Uche alibeba bunduki kanisani ili atumie kama kielelezo juu ya kwa nini washiriki wa kanisa ‘wanahitaji kutumia bunduki na kutetea imani yao’.

Alipopanda mimbari kwa mara ya kwanza, washiriki wa kanisa walicheka kwa sura isiyo ya kawaida ya bunduki aliyoifunga kwa nyuma, lakini mchungaji huyo aliwambia “wasiondoke wakae walipo, nimekuja nikiwa tayari asubuhi ya leo kwa sababu nahitaji kulinda imani,” alisema huku akiinua bunduki juu kuwaonesha alichokuwa anamaanisha.

“Tunaishi katika nyakati ambazo tunahitaji kulinda imani yetu lakini tunahitaji kulinda imani yetu dhidi ya majambazi, maharamia na watu waovu ambao hawataki Mungu aongoze maisha yetu,” aliongezea.

Hata hivyo kuonekana kwa bunduki kanisani kuliwafanya watu kuwa na mjadala mkubwa katika mitandao ya kijamii, ambapo baadhi walitetea kitendo hicho na wengine walishangaa iwapo ni sawa kumiliki bunduki, au kuingia nayo kanisani kwa mahubiri. BBC

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages