NEWS

Saturday 25 February 2023

Mwenyekiti CCM Mara achangisha milioni 35.6/- kukamilisha nyumba ya Mchungaji Kanisa la SDA Tarime CentralNa Mara Online News
-----------------------------------

MWENYEKITI wa CCM Mkoa wa Mara, Patrick Chandi (wa tatu kutoka kushoto pichani juu), leo ameongoza changizo maalumu kwa ajili ya ukamilishaji wa nyumba ya Mchungaji wa Kanisa la Waadventista Wasabato (SDA) Tarime Central, ambapo kiasi cha shilingi milioni 36.5, zikiwemo fedha taslimu takriban milioni 29.

Katika tukio hilo, Chandi ameongozana na viongozi mbalimbali, wakiwemo Mjumbe Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM wa Mkoa wa Mara, Christopher Mwita Gachuma na Mjumbe wa NEC (Viti 3 UWT), Joyce Ryoba Mang’o.

Chandi ameeleza kufurahishwa na mapokezi aliyopata katika hafla hiyo - ambayo pia imehudhuriwa na Askofu wa Kanisa la SDA Jimbo la Mara, Mchungaji John Matongo ambaye ameongoza ibada iliyohudhuriwa na mamia ya watu katika kanisa hilo lililopo wilayani Tarime.

Awali, Chandi na msafara wake wametembelea mradi huo wa nyumba ambayo ujenzi wake umefikia hatua za ukamilishaji (finishing).

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages