NEWS

Sunday 19 March 2023

Jumuiya ya Wazazi CCM Tarime yawatunuku Kiles na Komote tuzo za heshima


Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Tarime, Samwel Mangalaya (kulia) akimkabidhi Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Simion Kiles cheti cha tuzo ya heshima.

Na Mara Online News
-----------------------------------

JUMUIYA ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Tarime imewatunuku Wenyeviti; Simion Kiles wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime na Daniel Komote wa Halmashauri ya Mji wa Tarime vyeti vya tuzo za heshima kutokana na michango yao ya hali na mali kwenye jumuiya hiyo na CCM kwa ujumla.

Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Samwel Mangalaya amewakabidhi vyeti hivyo wakati wa kikao cha baraza la Jumuiya hiyo kilichofanyika kwenye ukumbi wa ofisi za CCM mjini Tarime, leo Machi 19, 2023.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Tarime, Samwel Mangalaya (kulia) akimkabidhi Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Tarime, Daniel Komote cheti cha tuzo y heshima.

Kiles na Komote wameishukuru Jumuiya hiyo na kuahidi kuendelea kushirikiana na viongozi wa CCM, wakiwemo wabunge katika kusimamia utekelezaji wa ilani ya chama hicho tawala kwa maendeleo ya wana-Tarime kama si Taifa.

“Nitaendelea kushirikiana na viongozi wengine kazi isonge mbele, tutaendelea kuungana na wabunge wetu, Kembaki [Michael Kembaki wa Tarime Mjini] na Witara [Mwita Waitara wa Tarime Vijijini] kufanya kazi kwa kasi kubwa, hatuwezi kuwaangusha,” amesisitiza Kiles ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Nyakonga.

Naye Komote ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Nkende, kwa upande mwingine amewahimiza viongozi wote wa CCM kuendelea kuwambia wananchi juu ya miradi ya mendeleo ya kisekta inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.

Viongozi mbalimbali katika picha ya pamoja baada ya kikao hicho

Aidha, Wenyeviti hao wa Halmashauri wametumia nafasi hiyo pia kukemea mmomonyoko wa maadili miongoni mwa wana-CCM, hususan kundi la vijana wachache wanaowabeza viongozi wa chama hicho wilayani Tarime kwenye mitandao ya kijamii.

“Wabunge wetu wako imara ila kuna uchonganishi unaopita kati kati hadi kwa wenyeviti wa halmashuri. Tuwaheshimu wabunge, wenyeviti wa halmashauri na madiwani wetu wote, lakini pia tushirikiane katika kutoa maamuzi,” Kiles amesema.

#Tunakuhabarisha Ukweli kwa Weledi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages