NEWS

Tuesday 7 March 2023

Madiwani Tarime Vijijini wapitisha bajeti ya TARURA kiasi cha shilingi bilioni 6.4 kwa mwaka wa fedha 2023/2024, Mhandisi Marwa atoa nenoNa Mara Online News
----------------------------------

BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime (Vijijini) limeidhinisha bajeti ya shilingi bilioni 6.4, ikiwa ni makisio ya mapato na matumizi ya Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) katika wilaya hiyo kwa mwaka wa fedha 2023/2024.

Hayo yamejiri katika kikao cha baraza hilo kilichofanyika katani Nyamwaga leo Machi 7, 2023.

Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kikao hicho kumalizika, Meneja wa TARURA Wilaya ya Tarime, Mhandisi Charles Marwa alisema bajeti hiyo itagusa sehemu kubwa ya vipaumbele vya matengenezo ya barabara vilivyowasilishwa na madiwani.

“Bajeti yetu ni shirikishi, madiwani walileta vipaumbele na sisi tukatembelea [maeneo husika], tukachakata na mwisho tukapanga pamoja, na leo wamehitimisha kwa kupitisha kile ambacho tumepanga kwa pamoja,” amesema.
Mhandisi Marwa akiwasilisha bajeti ya TARURA

Hata hivyo Mhandisi Marwa amesema hawakuingiza vipaumbele vyote vilivyowasilishwa na madiwani kutokana na ufinyu wa bajeti.

“Hatujagusa vipaumbele vyote vilivyowasilishwa kwa sababu mahitaji ni mengi ukilinganisha na bajeti, lakini kwa sababu kupanga ni kuchagua, na Roma haikujengwa kwa siku moja - basi hata hiki ambacho tumekipitisha leo naamini kikija tutakisimamia vizuri na kitatoa matokeo chanya ambayo yatagusa jamii,” amesema meneja huyo wa TARURA.

#Tunakuhabarisha Ukweli kwa Weledi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages