NEWS

Wednesday 8 March 2023

Wafanyakazi wanawake Barrick North Mara waahidiwa fursa kemkem na mazingira bora zaidi kaziniNa Mwandishi Wetu, Nyamongo
------------------------------------------------

MGODI wa Dhahabu wa North Mara umeahidi kuendelea kuwapa wafanyakazi wanawake fursa zaidi, ikiwemo kuwapandisha nyadhifa na kuwaboreshea zaidi mazingira ya kazi.

Meneja Mkuu (GM) wa Mgodi huo, Apolinary Lyambiko amesema hayo leo Machi 8, 2023 kwenye maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani - ya wafanyakazi hao wa kike katika mgodi huo unaoendeshwa na Kampuni ya Barrick kwa ubia na Serikali ya Tanzania, kupitia Kampuni ya Twiga Minerals.

Lyambiko amesema Kampuni ya Barrick pia ina programu maalumu ya kuwapa wanawake kipaumbele katika suala la ajira na kuwajengea uwezo wa shughuli za uchimbaji madini.

Meneja wa Barrick Tanzania, Dkt Melkiory Ngido (katikati mbele), GM Lyambiko (kulia) na wengine wakijumuika kuimba na kucheza wakati wa maadhimisho hayo

Meneja huyo amesema idadi ya wafanyakazi wanawake katika mgodi huo imeongezeka uliganisha na miaka ya nyuma, na amewamiminia sifa kwamba wengi wao wanaonesha bidii na ufanisi mkubwa katika utekelezaji wa majukumu yao kazini.

“Takwimu za mwaka jana na sasa zinaonesha kuna ongezeko la wafanyakazi wanawake katika mgodi wetu, na wengi wao wanafanya kazi nzuri. Hivyo tutaendelea kuwapa fursa, siyo tu kujishughulisha na uchimbaji, bali na kuwamotisha pia,” amesisitiza GM Lyambiko na kuwataka kuendelea kuonesha uwezo mkubwa kazini na kujenga tabia ya kujiamini.

Sambamba na hayo, Meneja huyo amesema mgodi huo pia utaendelea kuboresha zaidi mazingira ya wafanyakazi wanawake, ikiwemo uboreshaji wa huduma zao wanapokuwa wamejifungua (maternity period).

Sehemu ya wafanyakazi wa mgodi wa North Mara wakiimba wimbo wa furaha wakati wa maadhimisho yao

Katika hatua nyingine, Lyambiko amesema suala la unyanyasaji wa kijisnia halikubaliki - akisisitiza kuwa linapaswa kuwa sifuri katika mgodi huo.

Amesema mtu yeyote atakeyeripotiwa kujihusisha na vitendo hivyo atawajibishwa mara moja, ikiwa ni pamoja na kufukuzwa kazi.

GM Lyambiko amesema hayo yote kujibu maombi mbalimbali kutoka kwa wafanyakazi wanawake katika mgodi wa North Mara yaliyowasilishwa kwake na Mwenyekiti wa wafanyakazi hao, Avemaria Bugulashi.

Mwenyekiti Avemaria akiwakilisha maombi ya wafanyakazi hao kwa uongozi wa mgodi

Kwa upnde wake, Meneja wa Barrick Tanzania, Dkt Melkiory Ngido amesema kampuni hiyo ina mpango mahususi wa kuwanua wafanyakazi wanawake katika migodi yake nchini, kupitia fursa za ajira, uongozi na mazingira bora.

“Msijisikie kuwa second class (daraja la pili), onesha kuwa mnaweza,” Dkt Ngido amesema katika maadhimisho hayo.

Dkt Ngido akizungumza katika maadhimisho hayo

Dkt Ngido (kulia) na GM Lyambiko (kushoto) wakiwalisha keki viongozi wa wafanyakazi wanawake wakati wa maadhimisho hayo

Awali, wafanyakazi hao wa mgodi wa North Mara wamefanya maandamano huku wakiwa wamebeba mabango yenye jumbe mbalimbai, zikiweo za kuomba kuboreshewa zaidi huduma, mazingira ya kazi na motisha kwa waliodumu muda mrefu kazini.


#Tunakuhabarisha Ukweli kwa Weledi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages