NEWS

Wednesday 1 March 2023

Mwenyekiti Halmashauri Wilaya ya Serengeti apongeza weledi wa gazeti la Sauti ya MaraNa Mwandishi Wetu, Serengeti
------------------------------------------------

MWENYEKITI wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti, Ayub Mwita Makuruma (aliyesimama pichani juu), amepongeza uongozi wa gazeti la Sauti ya Mara kwa kusimamia na kuzingatia maadili ya taaluma ya uandishi wa habari katika kutekeleza majukumu ya kuihabarisha na kuielimisha jamii.

Makuruma ametoa pongezi hizo wakati akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo cha robo ya pili ya mwaka 2023/2024, kilichofanyika mjini Mugumu leo.

Amesema chombo hicho cha habari kimekuwa kikiripoti habari za kweli, zilizofanyiwa utafiti wa kina, zisizoegemea upande mmoja na zinazoakisi kaulimbiu yake inayosema “Tunakuhabarisha Ukweli kwa Weledi”.

“Hata wanapopata taarifa inayohusu halmashauri hawasiti kuuliza viongozi husika ili kupata kauli ya upande wa pili, kwa mujibu wa maadili ya uandishi wa habari,” amesema Makuruma ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Busawe kwa tiketi ya chama tawala - CCM.

Kiongozi huyo ametumia nafasi hiyo pia kutoa wito wa kuhamasisha waandishi wa vyombo vingine kuiga mfano huo na kuepuka kuandika habari zisizo za kweli.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages