NEWS

Monday 20 March 2023

Rais Samia apokea Dola za Marekani milioni 30 kutoka Barrick za kujenga mabweni na madarasa ya kidato cha sita na tano nchiniRAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan (kulia), amepokea mfano wa hundi yenye thamani ya Dola za Marekani (USD) milioni 30 kutoka kwa Mtendaji Mkuu ambaye pia ni Rais wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation, Mark Bristow (kushoto), Ikulu Chamwino mkoani Dodoma leo Machi 20, 2023.

Fedha hizo ni kwa ajili ya shughuli mbalimbali za elimu, ambapo zitatumika kugharimia ujenzi wa mabweni 273 na vyumba vya madarasa 1,094 ya wanafunzi wa kidato cha tano na sita katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages