NEWS

Thursday 30 March 2023

Wananchi Nyanungu wachangamkia fursa ya uwekaji vigingi mpaka wa Hifadhi ya Serengeti


Sehemu ya milima ya Nyanungu

Na Mara Online News
---------------------------------

WANANCHI wa kata ya Nyanungu wilayani Tarime wameendelea kujitokeza kupata ajira za muda mfupi kwenye uwekaji wa vigingi vya mpaka wa vijiji vyao na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, kwa mujibu wa taarifa za uhakika kutoka eneo la tukio zilizoifikia Mara online News hivi punde.

“Yaani sasa hivi wananchi wanawahi ili wapate kazi ya kukoroga hata zege na kazi zingine, ingawa hata hivyo wengine wanakosa kazi,” amesema mkazi wa kata hiyo aliyejitambuslihsa kwa jina la Mniko.

Aidha wananchi hao wameanza kujenga mahusiano mazuri na wataalamu wa Serikali wanaoshiriki shughuli za usimikaji wa vigingi hivyo - ambazo leo zimeingia siku ya nne mfululizo.

“Wataalamu walikuwa na hofu lakini sasa hivi wameanza kuzoeana na wananchi. Baadhi ya wananchi wanawauzia miwa na vitu vingine,” ameongeza Mniko.

“Jana mvua ilinyesha nyingi lakini hali ni shwari na kazi inaenda vizuri, wananchi wanajitokeza kuomba kazi wenyewe, tunataka maendeleo, tumechoka na hali ya kuwa nyuma miaka yote,” amesema mkazi mwingine wa kijiji cha Kegonga aliyejitambusha kwa jina la Godfrey Marwa.

Kwa upande mwingine, wananchi hao wameeleza kushangazwa na wanasiasa wakiwemo viongozi wa kuchaguliwa wanaojaribu kugeuza mpango huo wa Serikali kuwa mtaji wa kujipatia umaarufu na maslahi yao binafsi.

“Hapa [Nyanungu] hakuna shida kama inavyoelezwa huko kwenye mitandao. Kazi inaendelea vizuri,” Marwa ameimbia Mara Online News kwa njia ya simu kutoka kijijini Kegonga.

Vyanzo vya uhakika kutoka serikalini vinasema kazi hiyo ya uwekaji vigingi vya mpaka inaendelea vizuri na kwa umakini wa hali ya juu.

Mkuu wa Mkoa wa Mara, Meja Jenerali Suleiman Mzee alizindua uwekeji wa vigingi hivyo Jumatatu wiki hii [Machi 27, 2023] na kuonya vikali wanasiasa kuacha kupotosha wananchi kuhusu mpango huo wa Serikali.

#Tunakuhabarisha Ukweli kwa Weledi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages