NEWS

Thursday 25 May 2023

Madiwani Serengeti watoa mrejesho wa utekelezaji miradi ya maendeleo, Mwenyekiti Makuruma ahimiza ukusanyaji mapato ya halmashauri

Mwenyekiti wa Halmashauri Wilaya ya Serengeti, Ayub Mwita Makuruma akizungumza kikaoni.


Na Godfrey Marwa, Serengeti
----------------------------------------------

MADIWANI wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti mkoani Mara wamewasilisha taarifa za utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika kata zao, wakitaja mafanikio na changamoto zilizopo.

Hayo yalijiri katika kikao cha baraza la madiwani hao kilichofanyika mjini Mugumu jana Alhamisi, kikiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Ayub Mwita Makuruma.

Madiwani kikaoni

Akifungua kikao hicho, Makuruma ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Busawe aliendelea kuhamasisha madiwani kusimamia utekelezaji wa shughuli za maendeleo, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha mapato ya fedha za halmashauri yanakusanywa kikamilifu katika kata zao.

Hoja zilizotikisa kikao hicho ni pamoja na ukosefu wa maji salama, upungufu wa dawa, vifaa tiba, watumishi wa afya, elimu na nyumba zao, ubovu wa miundombinu ya barabara na huduma ya umeme katika baadhi ya maeneo.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri, Victor Rutonesha akizungumza katika kikao hicho.

Akijibu hoja za madiwani, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri, Victor Rutonesha alisema serikali inaendelea na juhudi za ufumbuzi wa changamoto zilizopo ili kuboreshea wananchi huduma za kijamii.

#Tunakuhabarisha Ukweli kwa Weledi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages