NEWS

Monday 22 May 2023

Mwalimu mbaroni kwa mauaji ya mwanafunzi NyanunguNa Mara Online News
-----------------------------------

JESHI la Polisi linamshikilia Mwalimu Chule kwa tuhuma za kumuua mwanafunzi wake, Ghati Mataro Tembo (14) wa darasa la tano katika Shule ya Msingi Mangucha iliyopo kata ya Nyanungu wilayani Tarime, Mara.

Taarifa zinadai mwalimu huyo alimpiga mwanafunzi huyo kwa fimbo  shuleni hapo jana Jumatatu.

Vyanzo vyetu vya uhakika kutoka serikalini vimearifu kuwa mwalimu huyo alitiwa mbaroni muda mfupi baada ya kutenda tukio hilo.

“Mwanafunzi huyo alifikwa na mauti muda mfupi baada ya kufikishwa katika Kituo cha Afya Masanga,” alisema mtoa taarifa.

#Tunakuhabarisha Ukweli kwa Weledi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages