NEWS

Tuesday, 18 July 2023

Barrick North Mara, Tarime Vijijini wajadili Kanuni mpya za Wajibu wa Wamiliki wa Leseni za Madini kwa Jamii kuhusu utekelezaji miradi ya CSR

Baadhi ya viongozi na wafanyakazi wa vitengo mbalimbali kutoka Mgodi wa Dhahabu wa Barrick North Mara na Halmashauri ya Wilaya ya Tarime (Vijijini) wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kushiriki kikao cha kujadili Kanuni mpya za Wajibu wa Wamiliki wa Leseni za Madini kwa Jamii kuhusu utekelezaji wa miradi ya CSR. (Picha na Christopher Gamaina)
-----------------------------------------------------

Na Mwandishi wa
Mara Online News
-------------------------

MGODI wa Dhahabu wa Barrick North Mara na Halmashauri ya Wilaya ya Tarime (Vijijini) wamekutana kujadili Kanuni mpya za Wajibu wa Wamiliki wa Leseni za Madini kwa Jamii za Mwaka 2023, kuhusu utekelezaji wa miradi chini ya mpango wa Uwajibikaji kwa Huduma za Kijamii (CSR).

Kanuni hizo zimeainishwa kwenye Tangazo la Serikali Na. 409 la tarehe 23/6/2023, Sheria ya Madini, Sura ya 123, zilizotengenezwa chini ya kifungu cha 129.

Wawakilishi wa Mgodi wa Barrick North Mara na Halmashauri ya Wilaya ya Tarime katika kikao kilichojadili kanuni hizo mjini Tarime leo Julai 18, 2023, ni viongozi na wafanyakazi wa vitengo mbalimbali, miongoni mwa viongozi wengine wa kijamii.


Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini, Mwita Waitara (aliyesimama kulia) akizungumza katika kikao hicho cha majadiliano. Aliyesimama kushoto ni Kaimu Meneja wa Idara ya Mahusiano wa Mgodi wa North Mara, Hermence Christopher Lulah.

Makala ya majadiliano ya kina juu ya kanuni hizo itachapishwa kwenye gazeti la Sauti ya Mara.

#Tunakuhabarisha Ukweli kwa Weledi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages