NEWS

Saturday, 1 July 2023

Mbunge Mtega afariki dunia kwa kugongwa na power tiller, Spika Tulia atuma rambirambi



Francis Leonard Mtega enzi za uhai wake

Na Mwandishi wa

Mara Online News
-------------------------

MBUNGE wa Jimbo la Mbarali, Francis Leonard Mtega amefariki dunia leo Julai 1, 2023 kwa ajali ya kugongwa na trekta dogo (power tiller) akiwa anaendesha pikipiki katika eneo la shamba lake Mbarali, mkoani Mbeya.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Tulia Ackson ametangaza kifo hicho, akieleza kusikitishwa nacho.

“Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Mhe. Francis Leonard Mtega. Natoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa, waheshimiwa wabunge na wananchi wa jimbo la Mbarali, Mwenyezi Mungu awape moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu,” amesema Spika Tulia.

Kupitia taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa Ofisi ya Bunge, Spika amesema ofisi yake kwa kushirikiana na familia ya marehemu inaratibu mipango ya mazishi, na taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.

#Tunakuhabarisha Ukweli kwa Weledi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages