NEWS

Monday 24 July 2023

Mwandishi mahiri wa habari wa BBC afariki dunia



GEORGE Alagiah (pichani), mmoja wa waandishi mahiri wa habari wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) waliofanya kazi kwa muda mrefu na wanaoheshimika zaidi, ameaga dunia.

Alagiah ambaye pia alikuwa msomaji wa habari amefariki dunia leo akiwa na umri wa miaka 67, miaka tisa baada ya kugundulika kuwa na maradhi ya saratani.

Taarifa kutoka kwa wakala wake imesema "alikufa kwa amani leo, akiwa amezungukwa na familia yake na wapendwa wake".

"George alipendwa sana na kila mtu aliyemfahamu, iwe ni rafiki, mfanyakazi mwenza au mwananchi. Alikuwa mtu wa kipekee,” imeongeza taarifa hiyo.

Alagiah alifariki mapema Jumatatu [leo], lakini "alipigana hadi mwisho wenye uchungu," wakala wake ameongeza.

Mkurugenzi Mkuu wa BBC, Tim Davie alisema "Katika BBC, sote tumehuzunika sana kusikia habari kuhusu George. Kwa wakati huu, tunaombea familia yake."

"George alikuwa mmoja wa waandishi wa habari bora na shupavu wa kizazi chake ambao waliripoti bila woga kutoka kote ulimwenguni na pia kuwasilisha habari bila dosari.

"Alikuwa zaidi ya mwandishi wa habari bora, watazamaji waliweza kuhisi wema wake, huruma na ubinadamu wa ajabu. Alipendwa na wote na tutamkosa sana."

Chanzo: BBC

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages