NEWS

Monday 24 July 2023

OCP Tanzania yaendesha mafunzo ya matumizi sahihi ya mbolea kwa wakulima kupitia AMCOS zinazosimamiwa na WAMACU


----------------------------------------------------
Na Mwandishi wa
Mara Online News
-------------------------

KAMPUNI ya OCP- Tanzania imeanza kuendesha mafunzo ya matumizi sahihi ya mbolea za ruzuku ya Serikali kwa wakulima na wananchi kwa ujumla katika Halmashauri za Mji wa Tarime na Wilaya ya Tarime (Vijijini) mkoani Mara.

Mafunzo hayo yanatolewa kupitia Vyama vya Mshingi vya Ushirika na Masoko (AMCOS) vinavyosimamiwa na Chama Kikuu cha Ushirika cha Wakulima wa Mara (WAMACU Ltd).

Akizungumza na Mara Online News mjini Tarime juzi, Afisa Kilimo kutoka OCP- Tanzania, Lucas Andrea Paul alifafanua kuwa mafunzo hayo yamejikita kwenye mbolea zinazotolewa na kusambazwa na kampuni hiyo.

Kampuni ya OCP- Tanzania imeanza kushirikiana na WAMACU Ltd kuuza na kusambaza mbolea kwenye AMCOS ili kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara.

Paul alitaja baadhi ya mbolea kuwa ni DAP yenye virutubisho muhimu vya Nitrogen na Phosphorus, ambayo inafaa kwa kupandia mazao ya mahindi, ndizi na maharage, miongoni mwa mengine.“Mbolea nyingine ni NPSZn yenye virutubisho vya Nikogen, Phosphorus, Sulfur na Zinc kwa ajili ya kupandia mazao kama vile mahindi, maharage na alizeti,” alisema Afisa Kilimo Huyo kutoka OCP- Tanzania.

Nyingine alisema NPSB yenye virutubisho vya Nitrogen, Phosphorus, Sulfur na Boron inayofaa kupandia na kukuzia mazao ya mahindi, alizeti, mpunga na maharage.

Alitaja mbolea nyingine kuwa ni NPK yenye virutubisho vya Nitrogen, Phosphorus, Potassium, Sulfur, Boron na Zinc ambayo matumizi yake ni kupandia na kukuzia mazao ya matunda na mbogamboga ikiwemo nyanya, viazi, karoti, hoho na kahawa.Kwa mujibu wa Paul, mbolea zote hizo zinapatikana katika ghala la WAMACU Ltd kwa bei ya ruzuku ya Serikali.

“Pia Kampuni ya OCP- Tanzania itaongeza upatikanaji wa mbolea nyingine za UREA, CAN na S.A,” alisema mtaalamu huyo wa kilimo.

#Tunakuhabarisha Ukweli kwa Weledi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages