NEWS

Sunday 30 July 2023

Shilingi milioni 56 zachangwa kupiga jeki ujenzi wa Kanisa SDA Turwa, ‘K’ Awashukuru wachangiaji


Na Mwandishi wa

Mara Online News

--------------------------

TAKRIBAN shilingi milioni 50 zimechangwa kupiga jeki ujenzi wa nyumba ya ibada unaoendelea katika Kanisa la Waadventista Wasabato (SDA) la Turwa lililopo mjini Tarime, Mara.


  Kiasi hicho cha fedha kilipatikana katika harambee iliyoongozwa na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara, Ghati Zephania Chomete kanisani hapo, jana.


  Mbunge huyo pamoja na marafiki zake kwa pamoja walichangia shilingi milioni 16.6.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri wa Wilaya ya Tarime, Simion Kiles alichangia shilingi zaidi ya milioni 17, huku kiasi kingine kikitolewa na waamini wa kanisa hilo pamoja na wageni wengine walioshiriki katika harambee hiyo.


   Viongozi wengine walioshiriki katika harambee hiyo ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara, Esther Matiko ambaye alichangia shilingi milioni mbili na Mbuge wa Jimbo la Tarime Vijijini, Mwita Waitara (shilingi laki tano).

  Kiles ambaye ni Mkuu wa Majengo katika Kanisa hilo aliwashukuru watu wote walioshiriki katika harambee hiyo - iliyofanyika sambamba na ibada ya hitimisho la makambi ya mtaa yaliyohudhuriwa na mamia ya wananchi wa mji wa Tarime na maeneo mengine ya mkoa wa Mara.


  “Napenda kuwashukuru wote walioshiriki kutuunga mkono katika harambee ya kuendeleza ujenzi wa nyumba ya ibada katika Kanisa la Turwa SDA,” Kiles ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Nyakonga kwa tiketi ya chama tawala - CCM, ameiambia Mara Online News leo.


  Mara Online News imefahamishwa kuwa jengo la kanisa litakalojengwa litakuwa la ghorofa.


 #Tunakuhabarisha Ukweli kwa Weledi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages