WATU wenye silaha wapatao 30 walivamia machimbo ya Nyabigena katika Mgodi wa Dhahabu wa North Mara baada ya kuruka ukuta usiku wa manane Alhamisi iliyopita, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kampuni ya Barrick, leo Julai 15, 2023.
Taarifa hiyo imeeleza kwamba walinzi wa kampuni binafsi ambao hawakuwa na silaha walijaribu kuwazuia wavamizi hao bila mafanikio, ndipo hatimaye wakalazimika kuomba msaada wa polisi ili kuwaondoa machimboni.
Katika tukio hilo, taarifa hiyo imesema mmoja wa wavamizi hao alijeruhiwa ambapo polisi walimpeleka hospitali iliyo karibu kwa matibabu, lakini baadaye kwa bahati mbaya mtu huyo alifariki dunia kutokana na majeraha.
Taarifa imeeleza kuwa mpaka sasa haijajulikana jinsi mvamizi huyo alivyojeruhiwa, na kwamba uongozi wa mgodi wa North Mara umeomba tukio hilo lifanyiwe uchunguzi.
No comments:
Post a Comment