NEWS

Monday 17 July 2023

Nyansaho achangisha shilingi milioni 92 harambee ya KKKT Usharika wa Serengeti


Mgeni rasmi, Mkurugenzi wa Biashara wa Benki ya Azania Tanzania, Rhimo Nyansaho (mwenye tai waliokaa) katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa KKKT Usharika wa Serengeti na wa Serikali wakati wa harambee ya kanisa hilo, jana.

-----------------------------------------------------

Na Godfrey Marwa, Serengeti

---------------------------------------

MKURUGENZI wa Biashara wa Benki ya Azania Tanzania, Rhimo Nyansaho amefanikiwa kuchangisha shilingi milioni 92 katika harambee ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Serengeti mkoani Mara.

Harambee hiyo ilifanyika jana kwa ajili ya kupata fedha za kugharimia ujenzi wa chumba cha darasa la shule ya awali, ofisi ya Usharika na ukumbi mdogo wa mikutano kanisani hapo.
Kutoka kulia ni mgeni rasmi, Rhimo Nyansaho, MC Jofrey Kitundu na Askofu Michael Adam wa KKKT Jimbo la Mara wakati wa harambee hiyo.

Nyansaho ambaye alikuwa mgeni rasmi, alichangia shilingi milioni 60, hivyo kuvuka lengo la harambee hiyo la kupata shilingi milioni 50.


Mgeni rasmi, Rhimo Nyansaho (mwenye miwani) wakati wa kukabidhi michango ya harambee hiyo.

Alitumia nafasi hiyo kuwahamasisha waumini wa kanisa hilo na Watanzania kwa ujumla kudumisha amani na upendo sambamba na kushirikiana na Serikali katika juhudi za kuliletea taifa maendeleo ya kisekta.

Chanzo: SAUTI YA MARA
#Tunakuhabarisha Ukweli kwa Weledi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages