NEWS

Thursday 10 August 2023

Lissu kutikisa Nyanungu, Sirari keshoTundu Lissu

Na Mwandishi wa
Mara Online News
------------------------ 

MAKAMU Mwenyekiti wa CHADEMA (Bara), Tundu Lissu anatarajiwa kuhutubia mikutano ya hadhara katika wilaya ya Tarime mkoani Mara kesho Ijumaa. 

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Mara, Lucas Ngoto, mikutano hiyo itafanyika kwa nyakati tofauti katika maeneo ya Nyanungu na Sirari. 

“Mhehimiwa Lissu atawasili Tarime kesho [Ijumaa] asubuhi na atafanya mikutano miwili; Nyanungu na Sirari,” Ngoto ameiambia Mara Online News na Gazeti la Sauti ya Mara kwa njia ya simu muda mfupi uliopita. 

“Natoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kumsikiliza Mheshimiwa Lissu,” amesema na kufafanua kuwa ziara hiyo ni mwendelezo wa Operesheni ya +255' inayoendeshwa na chama hicho kikuu cha upinzani Tanzania. 

#Tunakuhabarisha Ukweli kwa Weledi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages