NEWS

Saturday 12 August 2023

TRA yakanusha taarifa ya tozo ya kodi kwa bodaboda


Na Mwandishi wa
Mara Online News
-------------------------


MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imesema taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kwamba pikipiki zitaanza kutozwa kodi - siyo rasmi.

"Hivyo waendesha bodaboda na wananchi kwa ujumla mnajuzwa kuondoa wasiwasi na taharuki, na muendelee na shughuli zenu," ilieleza sehemu ya taarifa kwa umma iliyotolewa na TRA jana Agosti 11, 2023.

Awali, taarifa iliyosemekana kutolewa na mmoja wa maafisa wa TRA ilisema pikipiki za magurudumu mawili (bodaboda) zitaanza kutozwa kodi ya shilingi 65,000 kila moja, huku bajaj ikitozwa shilingi 120,000 kwa mwaka.

#Tunakuhabarisha Ukweli kwa Weledi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages