Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Mwanza, Gabriel Mugini (kulia) akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza.
---------------------------------------------------
Na Mwandishi Wetu –
Mara Online News, Mwanza
--------------------------------------
MAONESHO ya 18 ya Biashara ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) yameanza jijini Mwanza jana Ijumaa, ambapo yanatarajiwa kuhudhuriwa na kampuni zaidi ya 200 kutoka nchi mbalimbali.
“Maonesho haya yatahitimishwa Septemba 3, mwaka huu. Wafanyabiashaa watapata fursa ya kuonesha na kutangaza bidhaa zao,” Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara wa Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) Mkoa wa Mwanza iliyoandaa maonesho hayo, Gabriel Mugini amesema leo Jumamosi.
Mugini ametaja faida nyingine za maonesho hayo yanayofanyika kwenye viwanja vya Furahisha, kuwa ni uwepo wa fursa ya wafanyabisahara wa Tanzanania kutengeneza mtandao wa kibiashara na kampuni kutoka mataifa jirani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mbali na Tanzania, nchi nyingine zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki ni Kenya, Rwanda, Uganda, DR Congo, Burundi na Sudan Kusini.
Kaulimbiu ya maonesho hayo inasema “Mazingira Bora ya Biashara ni Kivutio cha Uwekezaji wa Biashara, Viwanda na Kilimo Afrika Mashariki.”
No comments:
Post a Comment