NEWS

Thursday 3 August 2023

Mchungaji KTMK asakwa kufuatia vifo vya watoto 14 Ziwa VictoriaMkuu wa Wilaya ya Bunda, Vicent Naano (mbele) akizungumza na wananchi kijijini Mchogondo jana, kuhusu hatua za serikali kufuatia ajali ya mitumbwi iliyosababisha vifo vya watoto 14 katika Ziwa Victoria.
----------------------------------------------

Na Mwandishi wa 
Mara Online News
-------------------------

MKUU wa Wilaya (DC) ya Bunda mkoani Mara, Vicent Naano amesema Jeshi la Polisi linamsaka Mchungaji wa Kanisa Takatifu la Mungu wa Kiroho (KTMK), kwa kutozingatia sheria na usalama wa waumini wake.

Jeshi hilo pia linawasaka wavuvi wenye mitumbwi iliyosababisha vifo vya watoto 14 katika Ziwa Victoria wakati wakitoka kusali kwenye kanisa hilo.

DC Naano alitangaza hatua hizo kijijini Mchigondo, Bunda jana, baada ya miili ya watoto 14 (wakike 12 na wa kiume wawili) kuopolewa ziwani, kukabidhiwa kwa familia husiku na kuzikwa.

Watoto hao walifariki dunia na watu wengine 14 (wanawake 10 na wanaume wanne) kuokolewa baada ya mitumbwi miwili iliyokuwa imewabeba kuzama katika Ziwa Victoria, wakati wakitoka ibadani huko KTMK, Jumapili iliyopita.

"Jeshi la Polisi limeanza kuwasaka wavuvi wenye hiyo mitumbwi, lakini pia linamsaka mchungaji wa kanisa hilo kwa kutozingatia sheria na kuhakikisha usalama wa waumini wake," alisema DC Naano na kuongeza kuwa kanisa hilo halina usajili.

Watoto waliofariki dunia katika ajali hiyo miongoni mwao walikuwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari.

#Tunakuhabarisha Ukweli kwa Weledi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages