NEWS

Tuesday 1 August 2023

Uhaba wa mafuta watikisa Tarime, Mugumu - Serengeti




Na Mwandishi wa
Mara Online News
------------------------


UHABA wa mafuta umeendelea kutikisa miji ya Tarime na Nyamongo mkoani Mara kwa takriban wiki moja sasa, huku baadhi ya madereva wa magari na pikipiki za abiria (bodaboda) wakidaiwa kulazimika kwenda kuyatafuta katika mji wa Isebania nchini Kenya. 

  Mara Online News imeshuhudia msongamano wa magari na bodaboda vikipambania kununua mafuta katika kituo kilichopo Bomani, baada ya kukosa huduma hiyo kwenye vituo mbalimbali mjini Tarime. 

  Madereva wa vyombo vya moto wamelalamikia hali hiyo, wakidai baadhi ya vituo katika miji hiyo vina mafuta lakini vinadanganya kuwa yameisha kwa lengo la kusubiri yapande bei ndipo waendelee kuuza. 

  “Mafuta yapo kwenye vituo ila hawataki kuuza kwa makubaliano ya kupandisha bei,” amedai mmoja wa wananchi hao. 

  Wafanyabiashara waliagiza mafuta kwa wingi - ghafla yakasuka bei kwenye soko la dunia ikafika mpaka nchini, wanaona wakiuza watapata hasara, hivyo wanasubiri bei ipande,” amedai mwananchi mwingine. 

  Tatizo la uhaba wa mafuta limeripotiwa pia katika mji wa Mugumu wilayani Serengeti, miongoni mwa maeneo mengine mkoani Mara.


Mara Online News itaendelea kukuhabarisha zaidi kuhusiana na tatizo hilo kadiri inavyopata taarifa mpya. 

#Tunakuhabarisha Ukweli kwa Weledi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages