NEWS

Tuesday 22 August 2023

Waziri Aweso amteua Nelly Msuya kuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji MWAUWASANelly Msuya

Na Mwandishi Wetu
----------------------------


WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso amemteua Nelly Msuya (pichani) kuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji (MD) wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA). 

Taarifa kwa umma iliyotolewa jana na Wizara ya Maji na kusainiwa na Mkuu wake wa Kitengo cha Mawasiliano, Florence Temba, ilisema Waziri Aweso amefanya uteuzi huo kwa mamlaka aliyo nayo kupitia Sheria Namba 5 ya Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira ya Mwaka 2019. 

Katika hatua hiyo, Nelly ameelekezwa kusimamia ukamilishaji haraka wa mradi wa maji utakaoongeza upatikanaji wa huduma ya majisafi kwa wakazi wa jiji la Mwanza. 

Siku moja kabla ya uteuzi huo wa Nelly kutangazwa, Waziri Aweso alitengua uteuzi wa Mhandisi Leonard Msenyele aliyekuwa MD wa MWAUWASA. 

#Tunakuhabarisha Ukweli kwa Weledi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages