NEWS

Monday 11 September 2023

Mbunge Chege alivyopamba ufungaji kambi la mafunzo ya UVCCM Rorya, awahamasisha waunda kikundi cha ushirika



Mbunge Jafari Chege (katikati) akipongezwa na vijana wa UVCCM Wilaya ya Rorya wakati wa shamrashamra za kufunga kambi lao jana Jumapili.
----------------------------------------------

Na Mwandishi Wetu, Rorya
------------------------------------ 

MBUNGE wa Jimbo la Rorya mkoani Mara, Jafari Chege ameshiriki hafla ya kufunga rasmi kambi la mafunzo kwa vijana wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Rorya. 

Mapema kabla ya kufunga kambi hilo katani Kirogo wilayani hapa jana, Chege alishiriki mazoezi kadhaa yakiwemo ya mbio na vijana wa umoja huo. 

Vijana hao walisikika wakiimba nyimbo za kuonesha kumkubali mbunge huyo kijana anayetokana na chama hicho tawala. 

Mbunge Chege (katikati mstari wa mbele) akishiriki mazoezi ya kukimbia

Pamoja na mambo mengine, Mbunge Chege aliwapatia vijana hao mchango wa nauli, ng’ombe mmoja na kuchangia shilingi 500,000 kwa ajili ya kuunda kikundi cha ushirika wao wa kiuchumi. 

Mbunge Chege ndiye aliyewahamasisha vijana hao kuunda kikundi hicho kwa ajili ya kujikita kwenye kilimo, ufugaji na uvuvi kwani ndizo shughuli kuu za kiuchumi zilizopo wilayani hapa. 

Aidha, mbunge huyo alishiriki kusimamia hatua za upatikanaji wa viongozi wa kikundi hicho -utakaokuwa chini ya usimamizi wa UVCCM Wilaya ya Rorya. 

Aliwashauri vijana hao kupitia kikundi hicho kuanza maandalizi ya kilimo cha mahindi katika bonde la mto Mara, akisema kwa sasa soko la mahindi ni kubwa ndani na nje ya wilaya hiyo. 

Hata hivyo, Mbunge Chege aliwakumbusha kuepuka kuchanganya siasa na shughuli za kikundi hicho cha ushirika ili waweze kujijenga kiuchumi. 

Chanzo: SAUTI YA MARA
#Tunakuhabarisha Ukweli kwa Weledi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages