NEWS

Wednesday 13 September 2023

Namba Tatu: Nimeombwa kuendelea kuisemea CCM MaraSamwel Kiboye "Namba Tatu"

Na Mwandishi Wetu –
Mara Online News
--------------------------
 

ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mara, Samwel Kiboye “Namba Tatu” amesema ameombwa kuendelea kukisemea chama hicho tawala kama alivyokuwa akifanya kipindi cha uongozi wake. 

Akizungumza na Mara Online News mjini Tarime leo, Namba Tatu amedai kuwa wananchi wengi wamekuwa wakimfuata kumwomba kutozira kuisemea CCM mkoani Mara. 

“Wana-Mara wengi wananisihi sana nisizire... wananiomba kwamba hata kama sipo madarakani niendelee kukisemea chama katika mkoa wetu kama nilivyokuwa nikifanya zamani,” amesema Namba Tatu. 

Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo mstaafu, wana-Mara wana haki ya kuambiwa maendeleo makubwa ya kisekta yanayoletwa na CCM na Serikali yake inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan. 

“Mimi ni mkereketwa wa CCM, ninaunga mkono wana-Mara wenzangu kwamba utashi wa kisiasa unahitajika kukisemea chama chetu ili kiwe na msisimko mkubwa kipindi hiki cha kuelekea kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwakani,” amesema Namba Tatu. 

#Tunakuhabarisha Ukweli kwa Weledi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages