Mkuu wa Mkoa wa Mara, Said Mohamed Mtanda (katikati), akizungumza na walimu (hawapo pichani) wa Shule ya Msingi Nkende wilayani Tarime, leo Ijumaa.
-----------------------------------------
Mara Online News
---------------------------
MKUU wa Mkoa (RC) wa Mara, Said Mohamed Mtanda amewaomba walimu wa Shule ya Msingi Nkende wilayani Tarime kuwa watulivu, wakati uchunguzi kuhusu tukio la kushambuliwa kwa watumishi wenzao ukiendelea.
RC Mtanda ametoa kauli hiyo leo Ijumaa alipozuru shuleni hapo na kuzungumza na walimu hao, akiwa amefuatana na viongozi wa Chama cha Walimu ngazi ya mkoa na wilaya.
Siku mbili zilizopita liliripotiwa tukio la baadhi ya vijana wa CCM kuwashambulia watumishi wawili akiwemo mwalimu wa shule hiyo, wakati Kamati ya Siasa ya chama hicho ngazi ya wilaya ilipokuwa kwenye ukaguzi wa miradi ya maendeleo.
Katika ziara hiyo ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo, Kamati hiyo ya Siasa iliwashirikisha viongozi kadhaa wa serikali na wabunge wawili wanaotokana na CCM.
#Tunakuhabarisha Ukweli kwa Weledi
No comments:
Post a Comment