Na Mwandishi Wetu Dodoma
Katika kuimarisha uhusiano wa miongo mingi kati ya Tanzania na Marekani, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt Rhimo Nyansaho, jana Januari 21, 2026 alikutana jijini Dodoma na Kaimu Balozi wa taifa hilo nchini, Andrew Lentz, kubadilishana mawazo namna ya kukuza uhusiano huo.
Taarifa iliyotolewa kuhusu mazungumzo hayo ilieleza jinsi mataifa hayo mawili yalivyopania kuimarisha masuala ya ulinzi, usalama na uchumi kwa manufaa ya wananchi wa pande zote mbili.
Waziri Nyansaho aliishukuru serikali ya Marekani kwa kuendeleza ushirikiano wa kidiplomasia tangu miaka ya mwanzo ya uhuru.
Naye Kaimu Balozi Lentz aliahidi kuendeleza na kudumisha uhusiano baina ya mataifa hayo mawili.
Tanzania na Marekani zilianzisha uhusiano wa kidiplomasia tangu mwaka 1961 kufuatia misingi iliyowekwa na hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, na hayati Rais wa 36 wa Marekani, John F. Kennedy.




No comments:
Post a Comment