NEWS

Monday 11 September 2023

Watu watatu mbaroni kwa tuhuma za utapeli Tarime, DC Mntenjele awataka wananchi kujihadhari



Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Kanali Michael Mntenjele akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo Jumatatu.
----------------------------------------------

Na Mwandishi Wetu –
Mara Online News
-------------------------- 


WATU watatu wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Polisi Tarime Rorya kwa tuhuma za utapeli wa kutoa ajira na kuuza dawa za asili. 

Kwa mujibu wa habari zilizothibitishwa na Jeshi la Polisi na Mkuu wa Wilaya (DC) ya Tarime, Kanali Michael Mntenjele leo Jumatatu, watu hao na wenzao kadhaa wanaojitambulisha kuwa ni viongozi wa Shirika la Alliance in Motion Global wamekuwa wakifanya utapeli huo kwa wananchi mbalimbali mjini Tarime. 

Waliokamatwa kwa tuhuma hizo na kufunguliwa jarada la ushunguzi Polisi wametajwa kuwa ni Anord Anthony Twamara (20), Emmanuel Musa Seleman (23) na Hezbon Tumwesiga Goodluck (20).


Katika mazungumzo na waandishi wa habari ofisini kwake leo Jumatatu, DC Mntenjele ametoa wito kwa wananchi kujihadhari na utapeli wa aina hiyo. 

#Tunakuhabarisha Ukweli kwa Weledi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages