NEWS

Tuesday 3 October 2023

Kamishna wa Uhifadhi Mwakilema ateuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya, Bajuta aondolewa Mamlala ya Hifadhi ya NgorongoroWilliam Simon Mwakilema

Na Mwandishi Wetu
-----------------------------


RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, amemteua Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), William Simon Mwakilema kuwa Mkuu wa Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga. 

Mwakilema anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jokate Mwegelo aliyeteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa jumuiya ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT). 

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Zuhura Yunus leo Jumanne, pia Rais Samia amemteua Naibu Kamishna wa Huduma TANAPA, Musa Kuji kuwa Kaimu Kamishna wa Uhifadhi wa TANAPA. 

Pia amemteua Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro, Elibariki Bajuta kuwa Mkuu wa Wilaya ya Urambo mkoani Tabora. 

Aidha, Mhe. Rais Samia ameteua na kufanya mabadiliko ya uteuzi kwa Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri na Makatibu Tawala. 

Baadhi yao ni Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga, Sixtus Raphael Mapunda ambaye amehamishiwa Wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam, kuchukua nafasi ya Mobhare Holmes Matinyi aliyeteuliwa na Mhe. Rais Samia kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari – Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali. 

Mwingine ni Mkuu wa Wilaya ya Urambo mkoani Tabora, Kenan Laban Kihongosi ambaye amehamishiwa Wilaya ya Momba mkoani Songwe, kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Fakii Raphael Lulandala aliyeteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM).

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages