NEWS

Thursday 26 October 2023

Mamba aua mvuvi mto Mara, mwenzake anusurika



Mamba

NA SAMSON CHACHA, Tarime
-------------------------------------------


MKAZI wa kijiji cha Kembwi wilayani Tarime, Juma Sasi Soronyo (40), ameuawa kwa kuliwa na mamba, huku mwenzake, Nyundo Ongwechi akinusurika wakati wakivua samaki katika mto Mara. 

Wakizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Kembwi, Mwita Jacob na Mwenyekiti wa Muungano wa Jamii Tarime Rorya, Okoyo Kamata walithibitisha kutokea kwa tukio hilo, 

Naye Diwani wa Kata ya Manga, Stephen Gibai alisema: “Tumepata msiba wa mkazi wa kijiji cha Kembwi, Juma Sasi Soronyo kuuawa na amba wakati wakivua samaki.” 

“Kumekuwa na matukio ya mara kwa mara ya mamba kuua wakazi wa vijiji vilivyo jirani na mto Mara vikiwemo vya Kembwi, Nyarwana, Nyamerambalo na Komaswa,” Gibai aliongeza. 

Kwa mujibu wa viongozi hao, mvuvi huyo aliliwa na mamba kiwiliwili na kubakizwa kichwa na kifua.

Kutoka na hali hiyo, walisema msako dhidi ya mamba hao unaendelea kijijini Kembwi, kwani mbali na kuua watu, pia wamekuwa wakiua na kula mifugo kijijini hapo. 

“Tunaomba msaada kutoka kwa askari wanyamapori kufika kiijiji kwetu tuungane kuwasaka mamba hawa wanaotishia maisha ya wanakijiji,” alisema Mwenyekiti wa Kijiji, Mwita. 

Chanzo: Gazeti la SAUTI YA MARA 
#Tunakuhabarisha Ukweli kwa Weledi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages