
Na Mara Online News
--------------------------------
#Tunakuhabarisha Ukweli kwa Weledi
--------------------------------
WATU wawili wamefariki dunia na wengine wawili kujeruhuiwa baada ya kufunikwa na mawe katika mgodi wa wachimbaji wadogo wa Marera ulipo kijiji cha Kerende wilayani Tarime, Mara.
Taarifa za hivi punde kutoka eneo la tukio zinasema ajali hiyo imetokea leo Jumatano saa nne asubuhi.
“Mwili wa mchimbaji mdogo mmoja tayari umeletwa katika chumba cha kuhifadhi maiti hapa Nyamongo na mwingine amekimbizwa Mwanza sasa hivi kwa ambulance akiwa na hali mbaya, ila tumuombe Mungu maana ndugu zake wengi hapa wameshutuka sana,” mkazi wa Nyamongo ameiambia Mara Online News.
Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Kerende ulipo mgodi huo, Muniko Magabe amethibitisha kutokea kwa vifo vya wachimbaji wadogo wawili katika tukio hilo.
“Duara limeangukia watu hapa, waliofariki dunia ni wawili na wengine wawili wamekimbizwa hospitali,” Magabe ameiambia Mara Unline News kwa njia ya simu kutoka eneo la tukio alikokuwa akishiriki shughuli za uokozi.
#Tunakuhabarisha Ukweli kwa Weledi
No comments:
Post a Comment