NEWS

Wednesday 11 October 2023

Mkurugenzi Professor Mwera Foundation ateta na Waziri wa Elimu jijini DodomaWaziri wa Elimu, Prfo Adolf Mkenda (kushoto) na Mkurugenzi wa Professor Mwera Foundation, Hezbon Peter Mwera wakiteta jambo jijini Dodoma jana.
---------------------------------------------

Na Mwandishi Wetu, Dodoma
----------------------------------------


MKURUGENZI wa Professor Mwera Foundation (PMF), Hezbon Peter Mwera, jana alipata nafasi ya kubadilishana mawazo na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda wakati wa mkutano wamiliki wa shule zisizo za Serikali jijini Dodoma. 

Hezbon ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wakuu wa Vyuo vya Ufundi Kanda ya Ziwa, pia alipata nafasi ya kubadilishana mawazo na viongozi kadhaa wa wizara hiyo, akiwemo Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti Ubora wa Shule nchini, Ephraim Simbeye.
Taasisi ya PMF inamiliki na kuendesha Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Tarime na Shule ya Sekondari Tarime Mchanganyiko katika mji wa Tarime mkoani Mara. 

#Tunakuhabarisha Ukweli kwa Weledi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages