NEWS

Saturday 28 October 2023

Mwenyekiti wa CCM Mara - Chandi achangisha shilingi milioni 37.7 Sabasaba SDA



Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Patrick Chandi Marwa akivishwa skafu alipowasili na kupokewa katika Kanisa la SDA Sabasaba mjini Tarime mapema leo Jumamosi Oktoba 28, 2023.
---------------------------------------------

Na Mwandi Wetu, Tarime
Mara Online News
----------------------------


MWENYEKITi wa CCM Mkoa wa Mara, Patrick Chandi Marwa leo Jumamosi Oktoba 28, 2023 ameongoza harambee iliyofanikisha ukusanyaji wa shilingi milioni 37.7 katika Kanisa la Waadventista Wasabato la Sabasaba lililopo mjini Tarime mkoani humo. 

Katika harambee hiyo, Mwenyekiti Chandi amechangia shilingi milioni tano (cash) na kuungwa mkono na baadhi ya waumini wa kanisa hilo na hivyo kiasi hicho kuongezeka hadi shilingi milioni 5.7. Fedha zilizochangwa zitatumika kwa ajili ya maendeleo ya kanisa hilo.


Mwenyekiti Chandi (katikati) na viongozi wengine wakifuatilia jambo kanisani.

Katika sehemu ya hotuba yake, kiongozi huyo ametoa wito kwa waamini wa kanisa hilo na wananchi wa mkoa wa Mara kwa ujumla kuendelea kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali ya CCM chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika kililetea Taifa maendeleo ya kijamii na kiuchumi. 

“Tuendelee kuiunga mkono Serikali kwa kazi kubwa na nzuri inayofanya, ndio maana hata mimi Mwenekiti wa chama tawala nipo hapa leo,” amesema Chandi ambaye anatajwa kuwa miongoni mwa wanasiasa watulivu, mahiri na wapenda maendeleo katika katika mkoa huo. 

Ibada hiyo ya changisho ilihudhuriwa pia na Mwenyekiti Kanisa la SDA Jimbo la Mara, Mchungaji John Matongo. 

#Tunakuhabarisha Ukweli kwa Weledi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages