NEWS

Sunday 29 October 2023

Dkt Mwita Mkami: Wasaidieni watoto watimize ndoto zao za maisha



Mhadhiri kutoka Taasisi ya TIA, Dkt Mwita Sospeter Mkami akikabidhi vyeti kwa Wahitimu wa Darasa la Saba wakati wa mahafali yao katika Shule ya Msingi ya Kidzcare iliyopo wilayani Bagamoyo, Pwani jana Oktoba 28, 2023.
------------------------------------

Na Mwandishi Wetu, Bagamoyo
-------------------------------------------
 

WAZAZI na walezi wametakiwa kuwa karibu na kuwasaidia watoto wao kutimiza ndoto zao katika maisha, kwa sababu watoto hukua kama wanavyolelewa. 

Wito huo ulitolewa jana Jumamosi na Mhadhiri kutoka Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Dkt Mwita Sospeter Mkami wakati wa Mahafali ya Darasa la Saba katika Shule ya Msingi ya Kidzcare iliyopo wilayani Bagamoyo, Pwani. 

Dkt Mkami ambaye ni 'PhD holder' alisema ndoto za wanafunzi haziwezi kutimizwa bila kuwepo msaada wa karibu kutoka kwa wazazi, au walezi wao. 


Dkt Mkami (wa pili waliokaa mbele) akiteta jambo na mmoja wa wageni

“Wazazi wangu, tuendelee kukumbuka kwamba shule ya kwanza na nzuri zaidi huanzia nyumbani, katika familia zetu. Lazima tusimame katika nafasi zetu,” alisema. 

Dkt Mkami, ambaye pia ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Mkoa wa Pwani, aliwahimiza wahitimu wa darasa la saba akisema: “Kama hamwezi kufanya vitu vikubwa, fanyeni vitu vidogo kwa usahihi.” 

“Ni matumaini yetu kwamba siku ya leo itakuwa mwanzo wa safari yenu katika kufanya vitu vidogo kwa usahihi. Baadhi yenu hapa ndiyo akina Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan wajao, Rais wa Jamhuri ya Muugano wa Tanzania. Wengine ndiyo mabilionea wajao kama vile Mohamed Dewji, Rostam Aziz, Said Salim Bakheresa na kadhalika, kwa kutaja wachache,” alisema Dkt Mkami. 

Shule ya Msingi ya Kidzcare imedhamiria kuwawezesha watoto kuwa watu wazima wanaojitegemea kifikra, wanaofanya maamuzi ya busara na ambao wanakua wakizingatia utu na maadili bila kujali utaifa, ukabila, dini au mazingira walikotoka. 

#Tunakuhabarisha Ukweli kwa Weledi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages