NEWS

Tuesday 3 October 2023

OCD Sirari SSP Chausiku awahimiza viongozi wa dini kuhubiri amaniOCD wa Sirari, SSP Chausiku akiwaelimisha viongozi wa dini kuhusu masuala ya ulinzi, usalama na amani leo Jumanne.
----------------------------------------------

Na Michael Nindi, Tarime Rorya
------------------------------------------
 

VIONGOZI wa madhehebu mbalimbali ya dini katika tarafa ya Inchugu wilayani Tarime, wamekumbushwa kuwa mabalozi wa kuhubiri amani katika nyumba zao za ibada na maeneo yanayowazunguka. 

Mkuu wa Polisi Wilaya (OCD) ya Kipolisi Sirari, SSP Chausiku Masasi amesisitiza hayo katika mkutano na viongozi hao wa kiroho - uliofanyika Sirari leo Jumanne. OCD Chausiku ametumia nafasi hiyo kuwaelimisha viongozi hao kuhusu ulinzi shirikishi, madhara ya vitendo vya ukatili wa kijinsia, matumizi ya dawa za kulevya, migogoro ya kifamilia na kujichukulia sheria mkononi. 


Katika mkutano huo, OCD Chausiku aliambatana na Afisa Operesheni Wilaya ya Sirari, ASP Feruzi na askari kata wa kata ya Mbogi, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Mtweve ambao nao walipata nafasi ya kuwasilisha mada mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages