NEWS

Thursday 19 October 2023

Polisi Sirari wakamata shehena ya bangi ikipelekwa sokoniMgunia ya bangi na pikipiki vilivyonaswa na Polisi Sirari
------------------------------------------

Na Mwandishi wa
Mara Online News, Tarime
----------------------------------------


KIKOSI cha kuzuia uhalifu katika Wilaya ya Kipolisi Sirari kimekamata magunia 26 ya bangi yakisafirishwa kwenda nchi jirani. 

Kwa mujibu wa taarifa zilizotufika hivi punde, bangi hiyo imekamatwa pamoja na pikipiki kadhaa zilizokuwa zikitumiwa kuisafirisha mapema leo Oktoba 19, 2023 katika kijiji cha Nyabisaga wilayani Tarime, Mara. 

Inadaiwa bangi hiyo imetoka katika kimojawapo cha vijiji vilivyo jirani na bonde la mto Mara ambalo vyanzo kutoka serikalini vinasema limegeuzwa kuwa eneo la kilimo cha zao hilo haramu - kulingana na sheria za Tanzania. 

Mara Online news inaendelea kumtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Polisi Tarime Rorya, Mark Njera kwa ajili ya kuzungumzia zaidi tukio hilo. 

#Tunakuhabarisha Ukweli kwa Weledi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages