NEWS

Monday 16 October 2023

WAMACU washinda Tuzo ya Usambazaji Bora wa Mbolea Kanda ya Ziwa

 


Na Mara Online News

-------------------------------

CHAMA Kikuu cha Ushirika cha Wakulima wa Mara (WAMACU Ltd), kimeibuka mshindi wa Tuzo ya Chama Bora cha Ushirika katika Usambazaji wa Mbolea Kanda ya Ziwa (pichani juu). 

Tuzo hiyo ilitoletwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mbolea Duniani, yaliyofanyika kitaifa mkoani Tabora, Oktoba 13, 2023. 

WAMACU Ltd ni miongoni mwa Vyama Vikuu vya Ushirika vilivyopewa dhamana ya kusimamia usambazaji wa mbolea za ruzuku kwa wakulima, kwa kushirikiana na Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB), TFC na OCP. 

Chama hicho kinajishughulisha na ukusanyaji wa kahawa kutoka kwa wakulima kwa ajili ya kuiongezea thamani na kuitafutia masoko ya nje. Pia kwa sasa kina leseni ya uwakala wa kusambaza pembejeo, ikiwemo mbolea kutoka TFRA. 

#Tunakuhabarisha Ukweli kwa Weledi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages