NEWS

Sunday 19 November 2023

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara apokewa Musoma Vijijini, akagua ujenzi wa jengo la ofisi ya CCM Wilaya
Na Mwandishi Wetu, Musoma
Mara Online News
------------------------------


MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mara, Patrick Chandi (wa 3 kushoto pichani juu), amewasili na kupokewa Musoma Vijijini leo Novemba 19, 2023 kuendelea na ziara yake ya kimkoa ya kuimarisha chama na kukagua maendeleo ya chama hicho tawala.

Baada ya kupokewa, Chandi ambaye amefuatana na wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa amekagua ujenzi wa jengo la ofisi ya CCM Wilaya Musoma Vijijini kabla ya kikao cha ndani.
Mwenyekiti Chandi (wa pili kulia) akikagua ujenzi wa jengo la ofisi ya CCM Wilaya ya Musoma Vijijini.
Jana Jumamosi, Mwenyekiti huyo alihitimisha ziara yake katika wilaya ya Butiama ambapo aliwaagiza viongozi wa wilaya hiyo kutatua kero za wananchi, na akapiga marufuku makundi ndani ya CCM.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages