NEWS

Saturday 18 November 2023

Chandi aanza ziara ya kukagua maendeleo ya CCM mkoani Mara



Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Patrick Chandi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja mbele ya jengo la ofisi ya CCM Tawi la Kitaramanka wilayani Butiama, leo Novemba 18, 2023 ambapo ameanza ziara ya kimkoa ya kukagua maendeleo ya chama hicho tawala.
-------------------------------------------------

Na Mwandishi Wetu, Butima

Mara Online News
-----------------------------


MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mara, Patrick Chandi amewasili katika wilaya ya Butiama kuanza ziara ya kimkoa ya kukagua maendeleo ya chama hicho tawala.

Chandi na msafara wake unauhusisha viongozi wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wamepokewa na Kamati ya Siasa Wilaya ya Butiama mapema leo Jumamosi Novemba 18, 2023.

Chandi (wa pili kushoto mbele) akikabidhi msaada wa saruji kuchangia ujenzi wa ofisi ya CCM Tawi la Kitaramanka wilayani Butiama.
Taarifa zinasema Mwenyekiti huyo atapita kila wilaya kukagua utelelezaji wa Ilani ya CCM ya Uchaguzi ya Mwaka 2020 - 2025.

Mara ni miongoni mwa mikoa inayoripitiwa kupewa mabilioni ya shilingi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbai ya maendeleo, fedha ambazo zainatolewa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongoza na Rais Samia Suluhu Hassan.
Mwenyekiti Chandi akivishwa skafu mara baada ya kuwasili na kupokewa wilayani Buriama kuanza ziara ya kimkoa ya kukagua maendeleo ya CCM mkoani Mara, leo Jumamosi Novemba 18, 2023.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages