NEWS

Sunday 26 November 2023

DAS Mwaisenye atia neno uwanja wa michezo wa ‘Shamba la Bibi’ TarimeKatibu Tawala wa Wilaya (DAS) ya Tarime, Mwl Saul Mwaisenye (katikati) akikabidhi mpira kwa Afisa Elimu Sekondari, Mwl Simbanilo Changiki wakati wa bonanza la michezo la kufunga mwaka na kumkaribisha DAS huyo, lililofanyika kwenye viwanja vya TTC mjini Tarime, leo Jumapili. (Picha na Mara Online News)
---------------------------------------------------------

Na Mwandishi wa Mara
Online News, Tarime
--------------------------------

Serikali wilayani Tarime, Mara imesema iko tayari kushirikiana na wadau wa michezo - hata katika juhudi za kutafuta wadhamini wa ukarabati wa uwanja wa michezo wa wilaya hiyo - unaojulikana pia kwa jina la Shamba la Bibi.

“Ofisi ya Mkuu wa Wilaya tuko tayari kutoa ushirikiano wa kutosha kwa mdhamini na wadau mbalimbali kufanya ‘levelling’ na kukarabati uwanja wa mjini Tarime,” amesema Katibu Tawala wa Wilaya (DAS), Mwl Saul Mwaisenye.

DAS Mwaisenye ametoa kauli hiyo wakati wa bonanza la michezo la kufunga mwaka na kumkaribisha wilayani Tarime, lililofanyika kwenye viwanja vya Chuo cha Ualimu Tarime (TTC), leo Jumapili.

Amesema michezo ni afya, ajira, biashara na huimarisha mahusiano na ujirani mwema, hivyo juhudi za pamoja zinahitajika katika kuiendeleza wilayani Tarime.

Aidha, katika kuonesha kuunga mkono michezo, kiongozi huyo ametoa shilingi 200,000 kwa ajili ya timu mbili za mpira wa miguu na shilingi 50,000 kwa waamuzi wawili.

Kwa upande wake Afisa Michezo na Utamaduni wa Halmashauri ya Mji wa Tarime, Tedd Musyangi ametumia nafasi hiyo kutoa wito wa kuwahimiza vijana kujenga tabia ya kujitokeza kushiriki michezo mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages