NEWS

Saturday 4 November 2023

DC Tarime asisitiza chakula kwa wanafunzi shuleni


Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Kanali Michael Mntenjele akisisitiza jambo kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, jana Ijumaa.
---------------------------------------

Na Godfrey Marwa, Tarime
Mara Online News
-----------------------------

MKUU wa Wilaya (DC) ya Tarime mkoani Mara, Kanali Michael Mntelenje amewahimiza wazazi na walezi kuhakikisha watoto wao ambao ni wanafunzi wa shule za sekondari na msingi wanapata chakula wawapo shuleni. 

“Kumekuwa na msisitizo wa mara kwa mara kuhusu utoaji wa chakula shuleni lakini bado tunafeli, maelekezo ya Serikali ni kwamba wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wapate chakula shuleni,” DC Mntenjele alisisitiza katika kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime kilichofanyika Nyamwaga, jana Ijumaa. 

Aliongeza: “Tunao wajibu wa kusimamia kile ambacho mtoto angekula nyumbani ndicho kipelekwe shuleni ili watoto wapate ugali au uji. Watendaji wa kata wakae vikao na kamati ya afya na lishe waelimishe wazazi juu ya jambo hili.” 


Wakati huo huo, baraza hilo la madiwani liliomba ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri kusimamia uharakishaji wa ujenzi wa stendi ya Ng’ereng’ere katika kata ya Regicheri ili ianze kufanya kazi na kuchangia pato la halmashauri hiyo.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Solomon Shati aliwaomba madiwani hao kuendeleza ushirikiano wa dhati katika kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya wananchi kwenye maeneo yao ya uongozi. 

Kikao hicho kilikuwa cha kuwasilisha taarifa za kata kutoka kwenye kamati za kudumu za Halmashauri ya Wilaya ya Tarime. 

#Tunakuhabarisha Ukweli kwa Weledi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages