NEWS

Saturday 11 November 2023

Mwenyekiti Halmashauri ya Serengeti aipa tano Serikali ya Awamu ya Sita, ajivunia mapato ya ndaniMwenyekiti Ayub Mwita Makuruma

Na Mwandishi Wetu, Serengeti
----------------------------------------


MWENYEKITI wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti mkoani Mara, Ayub Mwita Makuruma, ametoa wito kwa wananchi wa wilayani humo kuendelea kuiamini na kuiunga mkono Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suhulu Hassan, kwa kazi kubwa inayofanya kuwaletea maendeleo ya kisekta.

“Mapato ya ndani katika Halmashauri yetu ya Serengeti yanaendelea kuongezeka, na hata taarifa ya CAG inaonesha tuko vizuri,” Makuruma ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Busawe kwa tiketi ya chama tawala - CCM alisema katika kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo kilichofanyika mjini Mugumu juzi Alhamisi.


Sehemu ya madiwani kikaoni
Kikao hicho kilijadili taarifa za maendeleo kutoka kata za halmashauri hiyo, ambapo pia kwa kauli moja madiwani walitoa azimio la kuitaka Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kuiomba Serikali Kuu fedha zitakazosaidia kugharimia matengenezo ya barabara ambazo hazipitiki katika wilaya hiyo ambayo sehemu yake kubwa ni maeneo ya uhifadhi wa wanyamapori, ikiwemo Hifadhi ya Taifa Serengeti.

#Tunakuhabarisha Ukweli kwa Weledi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages