NEWS

Wednesday 22 November 2023

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara ziarani Serengeti



Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Patrick Chandi (kushoto) akipokewa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Serengeti, Morobanda Japan, miongoni mwa viongozi wengine, leo Novemba 22, 2023.
-----------------------------------------------------

Na Mwandishi wa Mara
Online News, Serengeti
--------------------------------


Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mara, Patrick Chandi amewasili na kupokewa na viongozi wa chama hicho wilayani Serengeti, kuendelea na ziara yake ya kuimarisha chama, kukagua maendeleo na kusikiliza kero za wananchi kwa ajili ya kuzitafutia ufumbuzi.

Mapokezi ya Chandi yameongozwa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Serengeti, Morobanda Japan, ambapo kiongozi huyo wa mkoa amekagua na kushiriki kwa vitendo ujenzi wa jengo la nyumba ya makazi ya Katibu wa CCM Wilaya, leo Novemba 22, 2023.


Chandi akishiriki kwa vitendo ujenzi wa jengo hilo.
Kisha Mwenyekiti Chandi amepata fursa ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la ofisi ya tawi la MCU, kabla ya kutembelea jengo la kitega uchumi cha CCM lililopo mjini Mugumu.


Mwenyekiti Chandi akivishwa skafu mara baada ya kuwasili wilayani Serengeti.

Mara Online News itaendelea kukuletea habari zaidi kuhusiana na ziara hiyo. Endelea kuwa nasi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages