
Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi (wa pili kushoto), akizungumza katika mkutano wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Tarime jana. Kulia ni Mkuu wa Wilaya, Meja Edward Gowele, miongoni mwa viongozi wengine.
Tarime
-------------
Mkuu wa Mkoa (RC) wa Mara, Kanali Evans Mtambi, ameitaka Halmashauri ya Mji wa Tarime kuwa na mkakati wa kuhakikisha taasisi zilizopo zinaondokana na matumizi ya kuni na mkaa, badala yake zijikite kwenye nishati safi.
Kanali Mtambi aliyasema hayo jana Jumanne, Juni 23, 2026 katika mkutano maalum wa Baraza la Madiwani wa halmashauri hiyo uliofanyika kujadili hoja za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka 2024/2025.
"Ninakutakeni kuweka mkakati mahususi wa nishati safi katika taasisi zinazotumia nishati za zamani, kwa kutumia mapato ya ndani na ruzuku kutoka Serikali Kuu na wadau mbalimbali.
"DC Meja Gowele jipange mshirikiane na wadau hao kuondokana na changamoto hizi, ninawafahamu vijana wengi hapa Tarime wanasaidia nje ya Mara,watumieni hawa wapenda maendeleo,” alisema Kanali Mtambi.

Madiwani kikaoni. (Picha zote na Mara Online News)
Kuhusu taarifa ya CAG, Mkuu wa Mkoa aliipongeza Halmashauri ya Mji wa Tarime kwa kupata hati safi.
Kwa upande wao, madiwani na watendaji wa halmashauri hiyo waliahidi kuendelea kushirikiana katika kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo na ukusanyaji wa mapato.
No comments:
Post a Comment